Frequently Asked Questions
Village Climate Solutions Limited (VCSL) receives many inquiries every day. To help you quickly find the information you need, we have answered some common questions below. Please review these FAQs before sending your message.
When does VCSL make payments to communities?
Payments are made after carbon credits are verified, sold, and revenues received. The first verification usually takes longer, but future payments are expected annually between July and December.
How long does verification take?
Usually several months, depending on project size, auditor schedules, and approval process. VCSL project is one of the large ones, and the first verification often takes longer.
Can any natural forest owner join VCSL?
No. Forests must demonstrate legal ownership, be older than 10 years, face real deforestation risk, and have long-term conservation potential.
Can I join if I own a small forest plot?
Eligible forests should generally be at least 500 hectares and located within our geographical reference region.
What happens if village forest is left outside the reserve?
It faces higher risks of encroachment, illegal harvesting, fire, and land conversion, which may lead to leakage.
Can woodlots with cashew, mango, teak or planted trees join?
No. VCSL focuses on natural forest carbon projects.
Can VCSL buy my land or forest?
No. VCSL works through partnerships, not land purchases.
Does VCSL own village forests it works with?
No. Ownership remains with communities or rightful landowners.
Can timber harvesting continue under carbon projects?
Yes, if harvesting is sustainably managed and strictly limited to no more than 1% of standing biomass annually.
Why does VCSL promote household dividends?
Because carbon credits are generated when communities choose conservation over forest-clearing agriculture; thus direct household benefits create stronger incentives for long-term forest protection. Also, the dividend model demonstrates the highest level of transparency and participation.
Does VCSL support evictions?
No. VCSL follows a no-eviction approach focused on education and incentives for deforestation agents.
How does VCSL ensure high-integrity carbon credits?
Through strong methods already aligned with VM0048 standards, independent verification, and transparent monitoring.
What makes VCSL carbon credits special?
They are aligned with conservative Verra VM0048 standards, deliver strong community and biodiversity benefits, target CCB Gold Level, and are designed to be ready for the CCP label.
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Village Climate Solutions Limited (VCSL) hupokea maswali mengi kila siku. Ili kukusaidia kupata taarifa haraka, tumejibu baadhi ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara hapa chini. Tafadhali pitia maswali haya kabla ya kutuma ujumbe wako.
VCSL hulipa jamii lini?
Malipo hufanyika baada ya krediti za kaboni kuthibitishwa, kuuzwa, na mapato kupokelewa. Uthibitishaji wa kwanza huchukua muda mrefu zaidi, lakini malipo ya awamu zinazofuata yanatarajiwa kati ya Julai na Disemba kila mwaka.
Uthibitishaji huchukua muda gani?
Kwa kawaida huchukua miezi kadhaa, kutegemea ukubwa wa mradi, ratiba za wakaguzi, na masharti ya idhini. Mradi wa VCSL ni miongoni mwa miradi mikubwa. Uthibitishaji wa kwanza mara nyingi huchukua muda mrefu zaidi.
Je, mmiliki yeyote wa msitu wa asili anaweza kujiunga na VCSL?
Hapana. Msitu lazima uwe na umiliki halali wa kisheria, uwe na zaidi ya miaka 10, uwe katika hatari halisi ya uharibifu, na uwe na uwezekano wa kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
Nina kipande kidogo cha msitu, naweza kujiunga?
Msitu unaostahili kwa kawaida unapaswa kuwa angalau hekta 500 na uwe ndani ya eneo letu la rejea la kijiografia.
Nini hutokea msitu wa kijiji ukiachwa nje ya hifadhi?
Huongezeka hatari ya uvamizi, uvunaji haramu, moto, na ubadilishaji wa matumizi ya ardhi, hali inayoweza kusababisha uvujaji.
Nina shamba la miti ya kupandwa, naweza kujiunga?
Hapana. VCSL inalenga miradi ya misitu ya asili pekee.
VCSL inaweza kununua ardhi au msitu wangu?
Hapana. VCSL hufanya kazi kwa ushirikiano, si kwa kununua ardhi.
VCSL inamiliki misitu ya vijiji inavyoshirikiana nayo?
Hapana. Umiliki hubaki kwa jamii au wamiliki halali.
Tunaweza kuvuna mbao tukiwa kwenye mradi wa kaboni?
Ndiyo, ikiwa uvunaji unasimamiwa kwa uendelevu na usizidi 1% ya uzitohai wa msitu kwa mwaka.
Kwa nini VCSL inahimiza gawio la kaya?
Kwa kuwa krediti za kaboni huzalishwa pale jamii zinapochagua uhifadhi badala ya kilimo kinachohusisha ukataji wa misitu, hivyo manufaa ya moja kwa moja kwa kaya huongeza motisha ya kulinda misitu kwa muda mrefu. Aidha, mfumo wa mgao wa gawio unaonesha kiwango cha juu zaidi cha uwazi na ushirikishwaji.
VCSL huhamasisha kufukuza wavamizi msituni?
Hapana. VCSL inahamasisha na kuhimiza wamiliki wa misitu iliyo kwenye mradi kutumia elimu pamoja na motisha kwa wahusika wa uharibifu wa misitu.
VCSL huhakikishaje ubora wa krediti zake?
Kupitia mbinu imara zinazozingatia viwango vya VM0048, uhakiki huru, na ufuatiliaji wazi.
Nini kinazifanya krediti za VCSL kuwa za kipekee?
Kuzingatia matakwa ya VM0048, manufaa kwa jamii, thamani ya bioanuwai, viwango vya CCB Gold Level, na utayari wa kupata lebo ya CCP.
Plot #245, Block B, Morocco
Ali Hassan Mwinyi Rd,
P.O. Box 4490,
Dar es Salaam – Tanzania
Meet our team
Plot #245, Block B, Morocco
Ali Hassan Mwinyi Rd,
S.L.P 4490,
Dar es Salaam – Tanzania
Fahamu timu yetu